BREAKING: Wagonjwa wa Corona Tanzania Wafika 254

Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema licha ya uwepo wa wagonjwa wapya 84 wa corona na kufanya visa vya corona kufikia 254 pia kuna vifo vipya vitatu vilivyotokea jijini Dar es Salaam vya watu waliothibitishwa kuwa na #COVID19 Hii inafanya idadi ya waliofariki kwa corona kufikia kumi.

 

Waziri wa Afya, ummy Mwalimu amesema wagonjwa hao wapya wa #CoronaVirus wamepatikana kuanzia Aprili 18 – Aprili 20 – Kati yao, Wagonjwa 68 wamepatikana Tanzania Bara na 16 huko Zanzibar

 

Dar es Salaam -33
Arusha -4
Mbeya -3
Kilimanjaro-3
Pwani -3
Tanga-3
Manyara-2
Tabora -1
Dodoma -3
Ruvuma -2
Moro- 2
Lindi-1
Mara-1
Mwanza -3
Mtwara -1
Kagera-1
Rukwa-2
Zanzibar-16.
Toa comment