Breaking: Wagonjwa wa Corona Wafikia 13 Tanzania

 

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu, amesema idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona imefikia 13 mpaka sasa ambao kati yao 8 ni Watanzania na 5 ni wageni mikoa ikiwa:

– Arusha 2

– Dar 8

– Zanzibar 2

– Kagera 1

Wagonjwa 12 wote waliambukizwa nje ya nchi na mmoja aliambukizwa na mmojawao kati ya hao 12.

 

“Mgonjwa wetu wa kwanza ambaye haturuhusiwi kutaja jina lakini alijitaja mwenyewe amepona COVID 19, tumepima sampuli mara tatu na zote zimeonyesha negative,tumeanza utaratibu wa kumruhusu kurudi nyumbani,” amesema Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Toa comment