Bwalya Apewe Kazi Mpya Simba

BOSI wa benchi la ufundi la Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck, amembebesha majukumu mazito kiungo wake Mzambia Rarry Bwalya la kuhakikisha anaonyesha kiwango kwenye mechi zao za ugenini baada ya kung’ara kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Kocha huyo amempa majukumu Bwalya na wachezaji wengine wa kikosi hicho kuhakikisha wanaonyesha uwezo mkubwa katika mechi zao za mkoani kwa ajili ya kuipa timu hiyo matokeo.Bwalya amekuwa mmoja wa viungo walioonyesha ufundi katika mechi mbili walizocheza dhidi ya Gwambina ambayo alianza na Biashara United Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba watacheza mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara Oktoba 4, dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.Mbelgiji huyo ameliambia Championi Jumatatu, kuwa anataka kuwaona wachezaji wake wote wakicheza kwa kiwango kikubwa kutokana na wengi kuwa na uwezo mkubwa.

 

“Wiki ijayo tunatoka kwenda ugenini dhidi ya JKT Tanzania, natarajia tutacheza hivihivi kwa kiwango kizuri hata kama kiufundi hatutacheza kama mechi iliyopita dhidi ya Gwambina.

 

“Lakini natarajia tunatakiwa kupambana kwa nguvu kama mechi zetu mbili zilizopita na uzuri ni kuwa tuna watu wengi wa kufunga mabao.”Bwalya alijiunga na Simba kwenye usajili huu akitokea Power Dynamos ya Zambia.

STORI: SAID ALLY, Dar es Salaam
Toa comment