Carlinhos! Alikataa Ofa ya Ulaya Akatua Yanga

IMEELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga na raia wa Angola, Carlos St’enio Fernandez ‘Carlinhos’,  amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno na badala yake ameamua kuja kukipiga Jangwani.

 

Yanga chini ya wadhamini wao Kampuni ya GSM, hivi karibuni ilifanikisha usajili wa mshambuliaji huyo aliyekuwa anakipiga Interclube ya nchini Angola ili kwa ajili ya msimu ujao.

 

Kwa mujibu wa Hersi, ujio wa mshambuliaji huyo Yanga umewashtua watu wengi Angola, kwani walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ureno.

 

“Ujio wa Carlinhos hapa Yanga umewashtua wadau wengi wa soka nchini Angola, kwani wengi walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ulaya na siyo Yanga.

 

“Hiyo ni kutokana na kiwango kikubwa ambacho anacho hivi sasa kwani ni kati ya wachezaji nyota wanaotazamwa Angola.  Amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno,” alisema Hersi.Toa comment