Carlinhos Apewa Kocha Maalum Yanga

BAADA ya kuona kuwa inaweza kuwa shida juu ya kuzungumza na wachezaji wenzake, staa wa Yanga, Muangola Carlos Carlinhos, amekabidhiwa kocha maalum na mabosi wake kwa ajili ya kurahisisha mazungumzo.

 

Mabosi wa Yanga wamepanga kumtumia aliyekuwa kocha wao msaidizi, Said Maulid, aliyewahi kucheza nchini Angola kwa ajili ya kuwa mtu maalum wa kumsaidia Carlinhos katika kufanya mazungumzo yake.

 

Carlinhos amejiunga na Yanga akitokea Interclube ya kwao Angola ambapo amekuwa akizungumza zaidi Kireno ambacho ndiyo lugha kubwa kwao.

 

Habari ambazo Championi limezipata ni kuwa, Maulid ambaye ni kocha wa timu ya vijana, ndiye ambaye amepangwa kuwa msaada katika kuwasiliana na Carlinhos baada ya kukaa Angola akiwa anaichezea Onze Bravos.

 

“Kwa kuwa Carlinhos imekuwa shida kwake kuzungumza Kingereza kwa sana kama ilivyo kwa wenzake, uongozi umeamua kumpa mtu maalum ambaye atakuwa msaada kwake katika kuzungumza.

 

“Uongozi umepanga kumtumia Said Maulid kwa sababu yeye alikaa na kucheza Angola, hivyo kujua lugha ya huko, hivyo ana uwezo wa kuzungumza naye na kusaidia juu ya mawasiliano yake akiwa hapa,” kilimaliza chanzo hicho.

 

 SAID ALLY, Dar es SalaamToa comment