Carlinhos Kumbe Amekataa Ofa Ureno

IMEELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga raia wa Angola, Carlos St’enio Fernandez ‘Carlinhos’ amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno na kuja kukipiga Jangwani.

 

Yanga chini ya wadhamini wao Kampuni ya GSM, hivi karibuni ilifanikisha usajili wa mshambuliaji huyo aliyekuwa anakipiga Interclube ya nchini Angola kwa ajili ya msimu ujao.

 

Carlinhos ni kati ya washambuliaji waliokuwepo kwenye mipango ya muda mrefu kusajiliwa na Yanga katika kukiimarisha kikosi chao kinachojiandaa na msimu mpya wa 2020/2021.

Kwa mujibu wa Hersi, ujio wa mshambuliaji huyo Yanga umewashtua watu wengi Angola, kwani walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ureno.

 

“Ujio wa Carlinhos hapa Yanga umewashtua wadau wengi wa soka nchini Angola, kwani wengi walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ulaya na siyo Yanga.

 

“Hiyo ni kutokana na kiwango kikubwa ambacho anacho hivi sasa kwani ni kati ya wachezaji nyota wanaotazamwa Angola, amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno.

 

“Carlinhos baba yake ni Mreno na mama yake ni Muangola, hivyo ni rahisi kwake kwenda kucheza kucheza soka huko Ureno,” alisema HersiToa comment