Carlinhos, Sarpong Wazoa Bil 2.5 Yanga

10 0Carlinhos, Sarpong Wazoa Bil 2.5 Yanga

ACHA kabisa yale mapokezi ya kishindo waliyofanyiwa mashine mpya za Yanga pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), taarifa ikufi kie kuwa, mashine hizo zote kwa jumla zimechota fedha za maana ndani ya klabu hiyo kutoka kwa mabosi wa timu hiyo.

 

Mastaa hao wakiwemo Muangola, Carlos Carlinhos na Mghana, Michael Sarpong, wanaunda kikosi cha Yanga kwa msimu ujao wa 2020/21 ambacho kina thamani ya Sh bilioni 2.5.

 

Mastaa wengine wapya ambao wamehusika katika kufi kisha thamani hiyo ya kikosi hicho ni Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Farid Mussa, Waziri Junior, Yassin Mustapha, Yacouba Sogne, Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomary, Zawadi Mauya na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema: “Maandalizi yote kuelekea siku ya kilele cha Tamasha la Wiki ya Wananchi yamekamilika ambapo kama kawaida yetu tumepanga kuhakikisha historia inaandikwa pale kwa Mkapa.

 

“Mashabiki wa Yanga wajiandae kushuhudia kikosi chenye thamani ya Sh. Bilioni 2.5 huku kikijikusanyia nyota kutoka mataifa nane tofauti ya Bara la Afrika ambao watauwasha moto.”

 

KOCHA MPYA ATUA, AANZA KAZI FASTA

Katika hatua nyingine, Bumbuli aliongeza kuwa, jana asubuhi walimpokea kocha mkuu wa kikosi hicho, Zlatko Krmpotic raia wa Serbia, huku akitarajiwa kuanza kazi leo Jumapili mbele ya Warundi, Aigle Noir katika mechi ya kirafi ki kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

“Kocha amewasili leo (jana) asubuhi na aliniambia ameshangazwa na mapokezi ya Kisinda (Tuisila) na Mukoko (Tonombe) walipokuja hapa nchini.“Kwa sasa tunafuatilia juu ya vibali vyake kwa ajili ya kuanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi chetu,” alimaliza Bumbuli.

 

Baada ya kocha huyo kutua, jana jioni alifi ka Uwanja wa Mkapa kushuhudia mazoezi ya kikosi chake ambacho leo Jumapili kitacheza mechi ya kirafi ki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.

 

Kocha huyo alifi ka uwanjani hapo wakati tayari kikosi cha timu hiyo kimeshafi ka ambapo aliomba muda kidogo wa kukaa na vijana wake na kuzungumza nao, kisha kuendelea na mazoezi.

 

Katika mazoezi, kikosi kilikuwa chini ya Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi, huku Mserbia huyo aliyechukua mikoba ya Luc Eymael, akikaa jukwaani na baadhi ya viongozi wa Yanga akiwemo Mwenyekiti, Mshindo Msola na Senzo Mazingisa.Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *