CCM: Wasanii watatu Belle9, Luludiva na Bonge la Nyau wamepata ajali tunafuatilia wapate matibabu haraka

11 0

Taarifa hiyo ya CCM imetolewa hii leo Septemba 7, 2020, na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Hamphrey Polepole kupitia ukurasa wake wa Twitter.

“Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa mshtuko taarifa za ajali mbaya ya gari iliyowahusisha wasanii Belle9, Luludiva na Bonge la Nyau, tunafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha wanapata huduma ya matibabu haraka na tunamwomba Mungu awape wepesi na kupona haraka”, imeeleza taarifa ya Polepole.

Wasanii hao wamepata ajali majira ya Alfajiri hii leo, katika eneo la Chalinze wakati wakitokea Iringa, huku chanzo wakieleza kuwa ni Lori kuwachomekea kwa mbele, ndipo dereva wao akalitumbukiza gari kwenye korongo ili wasigongane uso kwa uso.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *