CEO mpya Simba, Barbara Gonzalez afanya mazungumzo na Rais wa CAF

1 0

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez, amekutana na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad na kufanyanae mazungumzo.


CEO huyo amekutana na Rais Ahmad, alipofanya ziara kwenye makao makuu ya Shirikisho hilo yaliopo jijini Cairo Misri.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Simba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Rais huyo wa CAF, amempongeza Barbara kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo kubwa kwa ngazi ya klabu huku akimtaka kuitumia vema fursa hiyo ili awe mfano kwa wanawake wengine.

Kwa upande wake CEO huyo mpya wa Simba, amemshukuru Rais Ahmad na shirikisho zima kwa ujumla kwa mapokezi mazuri na kuahidi kufanya kazi kwa bidii.

Posted from

Related Post

KATUNI

Posted by - August 28, 2019 0
KIJIWE CHETU The post KATUNI appeared first on Gazeti la Dimba. Source link

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *