Chadema: Wenye Ushahidi wa Matumizi Mabaya ya Fedha Auweke Hadharani

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewataka Wabunge wenye ushahidi juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha kuuweka hadharani.

 

Hayo yamesemwa na Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, kufuatia wimbi la Wabunge waliotangaza kukihama chama hicho na kudai kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe anatumia vibaya fedha za chama.

 

Mei 22, 2020 Susan Maselle na Joyce Sokombi, Wabunge Viti Maalumu wa CHADEMA, walitangaza adhima ya kukihama chama hicho na kujiunga na NCCR-Mageuzi na kutoa shutuma kadhaa ikiwamo unyanyasaji wa kingono.

 

Pia, walidai hakuna mtu anayeruhusiwa kuhoji juu ya matumizi ya fedha za CHADEMA ambapo tuhuma hizo pia ziliwahi kutolewa Bungeni na Spika Job Ndugai na kumtuhumu Mbowe kuwa anawalazimisha wabunge kuchangia fedha hizo.

 

Aidha, Kamati Kuu ya CHADEMA imefanya kikao chake kwa njia ya kidijitali na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba katika mazingira ya uwepo wa #Corona, kupitia kikao hicho Mbowe kwa niaba ya CHADEMA amewatakia heri ya Eid Al Fitri Waislamu wote.Toa comment