Championi, Spoti Xtra Zaungana Kutokomeza Corona

 

GLOBAL Publishers kupitia magazeti yake bora ya michezo Tanzania ya Championi na Spoti Xtra, imeanzisha kampeni ya kuzuia kusambaa kwa Virusi vya Corona na kuvitokomeza kabisa.

 

 

Katika kampeni hiyo, leo Alhamisi timu ya Global Publishers ilitembelea mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuweka ndoo maalum za maji ambapo watu watakuwa wakinawa katika kujikinga na Corona.

Baadhi ya mitaa ambayo timu ya Global Publishers ilitembelea ni Kituo cha Daladala cha Makumbusho na Simu 2000 maarufu Mawasiliano.

 

Baada ya kuwekwa kwa ndoo hizo za maji, watu mbalimbali wakawa mstari wa mbele katika kunawa ili kuungana na Global Publishers kutokomeza Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

 

 

 

 

“Tumeamua kujitolea kuisadia jamii na Serikali kwa ujumla kupambana na ugonjwa wa Corona. Sisi ni sehemu ya jamii, tunajua umuhimu wa afya za wasomaji wetu, afya za wanamichezo na Watanzania kwa ujumla. Tuendelee kujikinga kwa kuwa ugonjwa wa Corona si jambo la utani,” Eric Shigongo, Mkurugenzi, Global Group.

 

PICHA | STORI NA IBRAHIM MUSSA | GLOBAL PUBLISHERS
Toa comment