Chelsea na Kai Havertz kumalizana ndani ya Saa 24 zijazo, Thiago Alcantara afanya maamuzi

7 0

Philippe Coutinho amerejea katika mazoezi akiwa ndani ya kikosi cha Barcelona kwa mara nyingine tena baada ya kuwatumikia kwa mkopo Bayern Munich.

Zikiwa zimepita siku 21 pekee tangu Mbrazil huyo kuisaidia Bayern kuibuka na ushindi wa jumla ya magoli 8-2 katika michuano ya Champions League mbele ya Barcelona na kupelekea kutwaa ubingwa Champions League pamoja na taji la Bundesliga.

Coutinho scored twice for Bayern Munich against Barcelona in the 8-2 thrashing

Mbrazi huyo ambaye alihusishwa na kuelekea Chelsea, Tottenham, Arsenal, Leicester na Newcastle ameonekana katika viunga vya Nou Camp akiwa na maski usoni inayomlinda dhidi ya virusi vya Corona.

Kai Havertz has left Germany's camp to seal his Chelsea deal , Bayer Leverkusen confirmed

Nyota wa klabu ya Bayer Leverkusen, Kai Havertz ameondoka katika kambi ya timu yake ya taifa ya Ujerumani kuelekea Chelsea ili kukamilisha dili lake la usajili lenye thamani ya paundi milioni 90.

Bayer Leverkusen imethibitisha kuwa kiungo huyo mshambuliaji kwa sasa yupo njiani kuelekea England ili kukamilisha mipango.

Frank Lampard is on the verge of securing another huge deal as he looks to battle for the title

Thiago Alcantara huwenda akaendelea kusalia Bayern Munich badala ya kuelekea Liverpool au Manchester United kama tetesi zilivyokuwa zina dai.

Thiago Alcantara admitted he would be happy to stay at Bayern, following Spain's 1-1 draw with Germany on Thursday night in Mercedes-Benz Arena

Thiago sasa amesisitiza kuwa kama hakuna ofa yenye kueleweka mezani atafurahi kuendelea kubaki Allianz Arena.

The Bayern star was instrumental in the club beating PSG in the Champions League final

Akizungumza baada ya sare ya goli 1 – 1 kwenye mchezo wa Hispania na Ujerumani nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 amekiambia chombo cha habari cha ZDF ”Kitu pekee ninachofikiria ni mchezo wetu dhidi ya Ukraine. Bayern ni nyumbani kwangu na ni mwenye furaha kuwa pale.”

Luis Suarez was spotted going to Lionel Messi's house on Thursday amid doubts over his exit

Luis Suarez ametembelea nyumbani kwa mchezaji mwenzake Lionel Messi hapo jana siku ya Alhamisi katika kiindi hiki ambacho maisha ya wawili hao ndani ya Barcelona yamegubikwa na wingu zito.

Messi akiwa katika mazungumzo na LaLiga kuhusiana juu ya hatima yake baada kuzua gumzo ya kutaka kuondoka Barcelona.

Wakati Suarez kwa upande wake akihusishwa kwenda kujiunga na miamba ya soka nchini Italia klabu ya Juventus. Mshambuliaji huyo wa taifa wa Uruguay ameoneka akiwa na mke wake Sofia Balbi nyumbani kwa Messi.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *