CHEMICAL: Nilimtongoza Mwanaume Akanikataa – Global Publishers

1 0CHEMICAL: Nilimtongoza Mwanaume Akanikataa

MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu yako pendwa ya My Style, kama ilivyo kawaida kila wiki huwa tunakutana hapa na kupiga stori mbili tatu na mastaa mbalimbali Bongo, ambapo tunapata nafasi ya kujua life Style yao mbali na kazi wanazofanya ikoje.

Leo tumefanikiwa kufanya exclusive interview na rapa mkali Bongo, Claudia Lubao ‘Chemical’ ambaye amewahi kutamba na nyimbo zake kama Am Sorry Mama, Tilalila, Asali, Unanifaa na nyingine kibao, amefunguka mambo mengi kuhusu maisha yake, uhusiano wa kimapenzi, nini anapenda kwa mwanaume na nini hapendi, ungana nami kwa mahojiano kamili:

My Style: Ratiba zako pindi unapoamka tu asubuhi huwa zipoje?Chemical: Kusema ukweli sina ratiba nzuri ambayo imenyooka, kwa sababu mara nyingi huwa nakuwa sipo nyumbani, nakuwa nipo bize na shughuli zangu zingine.

My Style: Mtu wa kwanza kufikiria kumpigia simu pale tu unapokurupuka kitandani, huwa ni nani?

 

Chemical: Nikiamka huwa naangalia kwanza time table yangu ili nijue naanza na kipi, lakini kuhusu simu inategemea nilitakiwa niongee na nani asubuhi hiyo.

My Style: Starehe yako kubwa ni nini?

Chemical: Napenda sana kuangalia tamthiliya.

My Style:Ukiwa na hasira sana, huwa unafanya nini?Chemical: Naondoka hiyo sehemu kwa sababu nakuwa sitaki kuendelea kumuona huyo mtu aliyeniudhi.

My Style: Jambo gani ambalo umewahi kulifanya ukiwa na hasira halafu baadaye ukajutia?

Chemical: Ni mambo mengi, nakumbuka nimeshawahi kumpiga mtu kibao halafu baadaye nikajutia kwa sababu sipendi ugomvi, pia nimeshawahi kuongea maneno mabaya kwa ajili ya hasira halafu baadaye nikajuta, lakini mwisho wa siku huwa naomba msamaha ili niwe na amani.

My Style: Kitu gani ambacho hakikosekani kwenye dressing table yako?

Chemical: Perfume, tissue na vitu vingine vya muhimu.

My Style: Nje na Tanzania, ni nchi gani nyingine ambayo huwa unapenda kwenda kula bata?

Chemical: Napenda kwenda

Portland kwa sababu kuna mazingira mazuri ambayo nayapenda kama ya Kilwa na Bagamoyo.

My Style: Una mpenzi?

Chemical: Hapana, nipo single.

My Style: Kwanini upo single?

Chemical: Sijapata wa kunifaa bado.

My Style: Haujapata kwa kuwa haupo tayari kwa kipindi hiki au wanaume wanaogopa kukufuata kwa sababu ya muonekano wako?

Chemical: Hapana, kwa sababu sidhani kama huu ni wakati sahihi kwangu kuwa na mpenzi, unajua ukiwa na mahusiano, maana yake akusaidie baadhi ya vitu, lakini mtu wa aina hiyo bado sijamuona, ndiyo maana nipo single.

Pia wanaume kuniogopa kwa sababu ya muonekano wangu, sijui lakini mpaka ikifikia hatua hiyo, inamaana huyo mwanaume hanifai tena.

My Style: Unatamani kuja kuingia kwenye ndoa siku moja?

 

Chemical: Kuhusu ndoa sijajua bado, lakini kuwa na mtu wa karibu ni kitu muhimu nitafikiria hilo, ila ndoa badobado kwanza.

My Style: Ikitokea ukatamani kuwa na mpenzi, ni tabia zipi ambazo utapenda mwanaume wako awe nazo?

Chemical: Anipende, anijali na anithamini basi, pia asiwe na mambo mengi.

 

My Style: Kitu gani ambacho huwezi kukibadilisha kwenye mwili wako kwa sababu ya mwanaume hata ikitokea umempenda sana?

 

Chemical: Yaani siwezi kubadilisha kitu chochote kwenye mwili wangu kwa sababu naamini mtu akikupenda, inamaana akupende jinsi ulivyo akianza kukubadilisha ili uwe kama anavyotaka, inamaana huyo mtu hakupendi.

 

My Style: Mwanaume wa aina gani ikitokea anakutaka kimapenzi hata iweje hauwezi kumkubalia?Chemical: Mwanaume anayevaa sana cheni, siwezi ku-date naye kwa kweli hata iweje.

 

My Style: Umeshawahi kuumizwa kwenye mapenzi?

Chemical: (Anacheka) Ndiyo lakini ilikuwa zamani sana kipindi hicho sijui hata maana ya mapenzi.

My Style: Umeshawahi kumtongoza mwanaume?

 

Chemical:Ndiyo, nimewahi.My Style: Vipi ulifanikiwa kumpata?Chemical: Hapana, alinikataa nikasema sitakuja kutongoza tena mwanaume.

My Style: Baada ya kukataliwa, ulijisikiaje?

Chemical: Kawaida kwa sababu hata hivyo nilikuwa najaribu bahati, lakini pia nilijikubali kwa sababu sio rahisi kwa mwanamke kueleza hisia zake kwa mwanaume lakini mimi nilijaribu.My Style: Umeshawahi kwenda kwa mganga?

Chemical: Hapana siamini katika waganga

.My Style: Ahsante sanaToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *