Chichi: Huduma ya ‘Msosi’ Iliniingiza Kwenye Sanaa

5 0Chichi: Huduma ya ‘Msosi’ Iliniingiza Kwenye Sanaa

Kwa wapenzi wa kufuatilia filamu za Kibongo, jina la Lilian Shirima maarufu kwa jina la ‘Chichi’, litakuwa sio geni masikioni mwenu. Mwanamama huyu mwenye shepu yenye mvuto wa kipekee, amejitengenezea jina kupitia filamu kadhaa nchini kwa kushirikiana na wasanii wakubwa kama vile Jacob Stephen ‘Jb’ Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengineo.

 

AMANI limezungumza naye ana kwa ana na kufunguka mambo mengi kuhusu kazi yake, aliingia vipi na mpaka sasa anafanya vitu gani.

 

Pia ameelezea jinsi alivyoweza kumbadilisha msanii wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Miss Bella’ na kuwa msanii mahiri kwa kuacha kufanya skendo zisizo na maana yoyote kwenye jamii. AMANI: Tueleze historia yako ya sanaa mpaka hapa ulipofika kwa ufupi.

 

CHICHI: Nakumbuka nilikuja Dar mwaka 2005, nikapata sehemu fulani hivi ya kufanya kazi ipo Kinondoni, ambapo wasanii wengi walikuwa wanapenda kuja kula hapo, mfano marehemu Steven Kanumba, Jb, Ray na wengineo.

 

Kwa hiyo mwisho wa siku, wakawa wananiona, nakumbuka mara nyingi walikuwa wananisifia kuwa mimi mzuri, hivyo nafaa kuigiza kuliko kufanya kazi pale, lakini nikawa nawapuuzia.

 

Lakini kuna baba alikuja ofisini kwangu na alikuwa ni mteja wangu sana, akaniambia kuna kazi anataka anipe, hivyo nitafute na wenzangu wawili, basi nikafanya hivyo.

 

Baadaye tukakutana sehemu akatufanyia mafunzo (training) kisha nikapita kwa ajili ya kwenda kwenye mkutano mkubwa wa kuchangia mfuko wa albino.

 

Kwa hiyo, kulikuwa na viongozi wengi wakubwa akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, ambapo nilipata nafasi ya kumhudumia, jambo ambalo wasanii wengine wakubwa waliikosa.

Huo ndiyo ukawa mwanzo wa mimi kujulikana kwa mastaa na kupewa kazi mbalimbali kwa ajili ya kuigiza. AMANI: Mpaka sasa umeshafanya filamu ngapi?

 

CHICHI: Nyingi sana… nimefanya filamu ya Nakwenda kwa Mwanangu, Vita Baridi, Tax Driver, The Woman of Principles, Uyoga na nyingine nimezisahau.

 

AMANI: Staa gani ambaye unashirikiana naye kwenye kazi mpaka sasa?

CHICHI: Msanii ambaye mpaka sasa nashirikiana naye kwenye kazi, ni Ndubagwe Misayo ‘Thea’ ambapo kwa sasa kuna tamthiliya tumecheza pamoja inaitwa Ndoa Yangu, inarushwa katika king’amuzi cha Star times.

 

AMANI: Kati ya hizo filamu zote ulizocheza, ipi ambayo ilikutambulisha rasmi kwa watu?

CHICHI: Filamu iliyo nitambulisha rasmi kwa watu, ni Tax Driver ya Jb.

 

AMANI: Umekuwa kwenye gemu ya filamu kwa muda mrefu sana, unaweza kutuambia unaionaje gemu ya filamu kwa sasa?

CHICHI: Filamu kwa sasa hivi zinalipa tofauti na zamani, lakini ulipaji wake sio sawa na jinsi ambavyo mtu akifanya tamthiliya, ndiyo maana unaona sasa hivi kila msanii anafanya tamthiliya.

 

AMANI: Sasa hivi wewe ni meneja wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva Isabela Mpanda ‘Miss Bella’, kwanza nataka kufahamu ilikuwaje ukajiingiza tena kwenye muziki?

CHICHI: Unajua ukishakuwa msanii, basi utafanya kila kitu ili upate chochote kitu, na mimi nimekaa kikazi zaidi sio kuuza sura.

 

AMANI: Ulikutana vipi na Miss Bella mpaka mkaingia makubaliano ya kufanya kazi pamoja?

CHICHI: Mimi na Bella tulikutana kwenye sanaa, tukafahamiana na mwisho wa siku tukawa marafiki, lakini sasa katika maongezi yetu, nikaona kuna fursa ya kufanya kazi pamoja, ndiyo ukawa mwanzo wa mimi kuwa meneja wake.

 

AMANI: Unafanya vitu vingi sana, wewe ni muigizaji, meneja wa msanii, mjasiriamali, mke na mama wa watoto kadhaa, lakini pia unaimba. Unawezaje kufanya vitu vyote hivyo kwa wakati mmoja?

CHICHI: Kila kitu ni malengo na jinsi ya kupangilia vizuri muda wako, nashukuru Mungu naweza kuyamudu yote hayo na watoto wangu wanasoma shule nzuri, lakini pia hivi karibuni niliachia wimbo wangu wa kumshukuru mama Samia unaitwa Mama Samia Simama Imara.

 

AMANI: Ugumu uko wapi kufanya kazi na Miss Bella?

CHICHI: Kabla sijaamua kuna fursa ya kufanya kazi pamoja, ndiyo ukawa mwanzo wa mimi kuwa meneja wake.

 

AMANI: Unafanya vitu vingi sana, wewe ni muigizaji, meneja wa msanii, mjasiriamali, mke na mama wa watoto kadhaa, lakini pia unaimba. Unawezaje kufanya vitu vyote hivyo kwa wakati mmoja?

CHICHI: Kila kitu ni malengo na jinsi ya kupangilia vizuri muda wako, nashukuru Mungu naweza kuyamudu yote hayo na watoto wangu wanasoma shule nzuri, lakini pia hivi karibuni niliachia wimbo wangu wa kumshukuru mama Samia unaitwa Mama Samia Simama Imara.

 

AMANI: Ugumu uko wapi kufanya kazi na Miss Bella?

CHICHI: Kabla sijaamua kufanya kazi na Bella, nilishamsoma na kumuelewa ni mtu wa aina gani, anapenda nini na nini hapendi. Hivyo, baada ya kujua yote hayo, ndipo nikaanza kufanya naye kazi.

 

AMANI: Miss Bella alikuwa na skendo nyingi mno mitandaoni, lakini sasa hivi amepunguza na haonekani tena akifanya mambo ya ajabu, umepambana kiasi gani kumrekebisha?

CHICHI: Bella alikuwa anakunywa pombe, kwa siku anaweza akamaliza hata kreti mbili za bia, lakini sasa hivi nikimuona anakunywa kiasi hicho, nagombana naye na kumuelekeza apunguze, hivyo nashukuru Mungu sasa hivi anakunywa mpaka bia mbili kwa siku.

 

Lakini pia mbali na hilo, nimemshirikisha sana kwenye maombi, hivyo sasa hivi Bella anamjua Mungu vizuri, ndiyo maana mnaona ametulia hana mambo mengi zaidi ya kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii ili afanikiwe.

 

AMANI: Miss Bella ni mtu wa aina gani kwa watu ambao wamezoea kumuona tu mitandaoni?

CHICHI: Sio fake, yaani anaishi maisha yake, akisema sina ni kweli hana na akiwa nacho, basi huwa ni mwepesi sana wa kusaidia wengine.

 

AMANI: Unahisi Miss Bella akiwekea kipaumbele kwenye mambo gani atafika mbali zaidi kisanaa?

CHICHI: Mimi naona aweke kipaumbele kwenye kufanya kazi kwa bidii, amuombe Mungu usiku na mchana, akifanya hayo atakuja kufanikiwa sana hapo baadaye.

Makala: Memorise Richard

 Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *