Chozi lamdondoka Suarez, awataka Barca wajipange (+Video)

1 0

Luis Suarez amejikuta akishindwa kuzuia hisia zake alipotakiwa kutoa neno moja tu la kwa heri kwa Barcelona mbele ya Kamera chozi lamdondoka na kumchukua dakika kadhaa kabla ya kurudi tena kwenye mazungumzo.

Suarez anaondoka Barcelona huku akiwa bado anahitaji kusalia hapo ila hana namna kwakuwa kocha mpya wa klabu hiyo Ronald Koeman amemtaka atafute pa kwenda.

Akitoa neno la mwisho kwa wachezaji wenzake aliyoishi nao pamoja Lionel Messi, Jordi Alba, Gerard Pique, Sergio Roberto na Sergi Busquets katika mahojiano ikiwa ndiyo safari imekwisha fika ya kwenda kukitumikia kikosi cha Atletico Madrid nyota huyo alitumia zaidi ya dakika kadhaa mpaka kuwa katika hali ya kuongea.

Suarez alijiunga na Barca mwaka 2014 akitokea Liverpool na ameisaidia kushinda mataji manne ya LaLiga, manne ya Copa del Rey na moja la Champions League mwaka 2015.

Suarez signed for Barcelona shortly after being banned for biting Italy defender Giorgio Chiellini at the 2014 World Cup

Nyota huyo ameishukuru klabu ya Barcelona huku akisema kuwa waliamu kumchukua licha ya kuwa kwenye skendo mbaya ya kumng’ata mtu katika kombe la Dunia lakini kwao hawakujali na walifanikisha kumsajili.

The Uruguayan was banned from all football-related activities for four months for the bite

”Klabu ilihitaji mabadiliko na kocha hajanijumuisha mimi katika kwenye wachezaji wake. Nahitaji kuonyesha kuwa ninaweza kuendela kuwa kwenye kiwango cha hali ya juu.”

Suarez anaamini Atletico inayo uwezo wa kushindana na Barcelona pamoja na Real Madrid kwenye michuano mbalimbali.

Barca walivyoniweka sokoni, simu nyingi sana zilipigwa zikiwa za ofa ya kunihitaji. Lani mimi nilihitaji timu ambayo nitaweza kushindana na Barcelona na Real Madrid.”

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *