Chuchu: Jaden Anapenda Kulipuka!

MSANII kunako Bongo Movie, Chuchu Hans amefunguka kuwa mwanaye ambaye amezaa na muigizaji mwenziye Vincent Kigosi ‘Ray’ anapenda sana kuvaa na kupendeza (kulipuka).

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Chuchu amesema kinachomshangaza ni kuwa, akimvalisha kawaida huwa analia, hapendi lakini akipigwa pamba za nguvu, anafurahia.

 

“Jaden anapenda sana kuvaa na hata nguo ambazo anataka kuvaa huwa anachagua yeye mwenyewe ndiyo maana hata mitandaoni anaonekana anapendeza, hiyo yote ni kwa sababu hiyo na ninamshukuru mwenyezi Mungu kwa sababu amepata ubalozi pale duka la nguo la Roby One Fashion na shopping zake namfanyia pale,’’ alisema Chuchu.

 
Toa comment