Corona: Mbowe Karantini Siku 14

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, sasa yupo karantini na amechukua hatua hiyo yeye mwenyewe na familia yake baada ya mtoto wake Dudley kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19). Kwa sasa Dudley anaendelea vizuri katika Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.

Mbowe amesema, amejiweka karantini jijini Dodoma huku akiendelea na shughuli pia kuwasiliana na watu wake kupitia mtandao na kwamba amechukua hatua hiyo ikiwa hatua madhibiti kusambaa na kusubiri majibu, kwamba kama naye ana maambukizi hayo ama la “nasubiri majibu kujua kama nina maambukizi ama la.”

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Kilimanjaro, amesema “unapokuwa na mgonja wa corona, jamii inakutazama kwa hofu na kwamba, kutokana na hivyo ni vema kujitenga kwa siku 14 huku nikisubiri majibu.”

Amesema, amekutana na watu wengi kabla ya kujiweka karantini, na kwamba ni jambo la kumuomba Mungu asiwe ameambukizwa.
Toa comment