Corona: Raia Wapigwa Risasi kwa Kukiuka Agizo la Rais

Watu wawili wamelazwa Hospitali Uganda baada ya kupigwa risasi na Polisi kwa kukiuka agizo la Rais Museveni, Alex Olyem na Kasim Ssebude wamepigwa risasi wakati wamepakizana kwenye Bodaboda ambazo zimepigwa marufuku ili kuzuia corona kuenea, mmoja amepigwa tumboni na mwingine mguuni.

 

“Alex na Kasim wamepigwa risasi kwa kubishana na askari, wanadai hawakufuatilia vyombo vya habari eti marufuku ya Bodaboda kupakiza abiria hawajaisikia, mwanzoni risasi zilipigwa juu wakawa wanakimbia zikapigwa tena mmoja ikampata mguuni mwingine tumboni, wamelazwa,” wamesema Polisi Uganda.

 
Toa comment