Corona Yamnyoosha Faiza

STAA wa Filamu ya Baby Mama, Faiza Ally ambaye ni mfanyabiashara anayefuata mizigo nje ya nchi, ameelezea namna janga la Virusi vya Corona lilivyomnyoosha.

 

Faiza ameiambia Bongo Selebriti ya Gazeti la IJUMAA kuwa, kwa sasa biashara imekuwa ngumu kwa sababu hawezi kusafiri kwenda kufuata mzigo kutokana na janga hilo.

 

“Corona ni hatari, watu wasichukulie poa kwa sababu mimi huwa ninakwenda China kuchukua bidhaa, lakini sasa siwezi kufanya hivyo kwa sababu ya Corona. Ninamuomba Mwenyezi Mungu atuepushe na balaa hili,” amesema Faiza ambaye ni mama wa watoto wawili.
Toa comment