Dah! Shaqiri akutwa na corona

4 0


MERSEYSIDE, England

XHERDAN Shaqiri anakuwa mchezaji wa tatu wa Liverpool kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona ndani ya wiki, kwani, ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa England wapo Thiago Alcantara na Sadio Mane.

Sasa, Shaqiri mwenye umri wa miaka 28 amekutwa na virusi vya corona baada ya kupimwa akiwa katika majukumu ya timu ya Taifa ya Switzerland.

Taarifa hiyo ilithibitishwa na Chama cha Soka cha Switzerland, itakumbukwa wiki imepita tangu Alcantara alipokutwa na maambukizi hayo kabla ya Mane.

Tangu ajiunge na Liverpool kutoka Bayern Munich, kiungo huyo raia wa Hispania alicheza mchezo mmoja dhidi ya Chelsea ambao aliingia kipindi cha pili.

Hata hivyo, alikosa mchezo wa Kombe la Ligi, Arsenal na ule ambao Liverpool walichapwa mabao 7-2 dhidi ya Aston Villa ndani ya Uwanja wa Villa Park.Source link

Related Post

Mr Nice: Muziki Pekee Unaua

Posted by - June 12, 2020 0
Mr Nice: Muziki Pekee Unaua June 12, 2020 by Global Publishers MSANII aliyejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Bongo…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *