Darleen: Tuna Uhusiano na Lukamba Lakini…

WIKI chache baada ya kuvuja kwa chati za mpiga picha wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Lukamba na dada wa msanii huyo, Queen Darleen zilizoashiria kwamba wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi, mrembo huyo ameibuka na kuanika ukweli wake.

 

Queen Darleen alisema, ni kweli wana uhusiano wa mtu na kaka yake lakini si wa kimapenzi kama watu wanavyosambaza mitandaoni.

 

“Mimi na Lukamba tuna uhusiano kwa sababu Lukamba ni kama kaka yangu kwa kuwa tunafanya kazi ofisi moja lakini hakuna kabisa mapenzi. Siwezi kuzuia, hiyo ni mitandao tu halafu mimi na Lukamba tumezoea kutaniana sana,” alisema Queen Darleen.

 

Katika sentensi nyingine, Queen Darleen alikanusha pia taarifa zinazozagaa mitandaoni kuwa ana ujauzito kwa kusema suala hilo halina ukweli.

 

“Ujauzito sina ni mambo tu hayo ya mita-ndao, mimi kama unav-yo-nio-na hapa sina mimba wala nini,” alisema Queen.

AMMAR MASIMBA

Toa comment