DC wa Kibaha, Bi Assumpter Mshana atinga ofisi za Osha na ujumbe huu (+Video)

14 0

Mkuu wa Wilaya Kibaha Mh Assumpter N. Mshama ameipongeza OSHA kwa kusimamia utekelezaji wa sheria ya Usalama na Afya Mahali pa kazi nchini kwa kufika sehemu kubwa wilaya humo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Ofisi za OSHA jijini Dar es salaam, Assumpter amesema ameamua kutembelea katika ofisi hizo ili kutoa pongezi kwa ushirikiano mkubwa walioupatia Wilaya hiyo kutokana zoezi la ukaguzi wa maeneo ya kazi hususani Viwanda vilivyopo Wilayani Kibaha kuona utekelezaji wa sheria ya usalama na Afya mahali pa kazi

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya, amewataka wamiliki wa Viwanda Wilayani Kibaha kuhakikisha wanazingatia sheria ya usalama na Afya Mahali pa Kazi, ili kulinda nguvu kazi, na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, katika ujenzi wa Viwanda.

Mshama ameongeza kuwa Katika kuunga juhudi hizo ambapo pia nchi za SADC zimemuunga mkono Mh Rais John Pombe Magufuli, katika zima za ujenzi wa Viwanda nchini.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi Khadija Mwenda, amesema wataendelea kusimamia sheria ya usalama na Afya kama sheria inavyoelekeza ili kuweza kulinda wafanyakazi katika maeneo ya kazi. Khadija amemshukuru mkuu huyo wa wilaya kuja kutembelea Ofisi za OSHA na kuwapa mrejesho juu ya zoezi maalamu la Ukagauzi lilofanywa na OSHA kwa lengo la kukagua maeneo ya kazi wilaya Kibaha kuona utekelezaji wa sheria ya usalama na Afya, kutokana na Wilaya hiyo kuwa na Viwanda Vingi hapa nchini.

Posted from

Related Post

Rais Magufuli afanya uteuzi

Posted by - November 29, 2020 0
Rais Dkt John Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *