De Bruyne Atwaa Tuzo, Aweka Rekodi City

KIUNGO wa Klabu ya Manchester City, Kevin De Bruyne ameibuka kuwa mchezaji bora wa Premier kwa msimu wa 2019/20, huku akiweka rekodi kuwa mchezaji wa kwanza ndani ya klabu hiyo kutwaa tuzo hiyo.

 

KDB ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwa na msimu bora ndani ya Premier akiwa amefunga ambao 16 na kutoa asisti 23 kwenye michuano yote. Kiungo huyo amesema hata yeye ameshangaa kwa kitendo cha kushinda tuzo hiyo tena akiwa mchezaji wa kwanza kutoka Man City.

 

“Ni kitu kikubwa kwangu, mimi kupigiwa kura nikiwa na wachezaji wengine na ushindani ukiwa mkubwa na kuchaguliwa kuwa bora ni jambo kubwa kwangu.

 

“Ila inashangaza kidogo kwani nimekuwa wa kwanza ndani ya City, licha ya wachezaji wengi bora kucheza ndani ya kikosi hiki kabla yangu na wengine bado wakiwa hapa, lakini sio mbaya kwani nimeiwakilisha klabu.

 

“Mimi kupigiwa kura na wengi ina maana kubwa wameona kuwa ninafaa na kuwa ni bora hivyo ni jambo la furaha kwamba nilikuwa na msimu bora.

 

“Kwa msimu uliopita siwezi kusema nilikuwa bora pekee bali nimekuwa bora wakati wote ambao nimekuwa nikicheza,” alisema KDB.

 

Wachezaji wengine ambao walitwaa tuzo hizo ni Pamoja na beki wa Liverpool, Trent Alexander Arnold aliibuka na tuzo ya mchezaji bora chipukizi, huku staa wa Manchester United, Marcus Rashford akipewa tuzo ya heshima kutokana na mchango wake kwa jamii kwa kusaidia watoto wenye uhitaji.Toa comment