Dembele kutua Manchester United – Bongo5.com

1 0

Manchester United wapo katika mazungumzo na miamba ya soka Barcelona juu ya uwezekano wa kufanikisha kumsajili, Ousmane Dembele.

Kwa mujibu wa Daily Record, vigogo hivyo vya soka kutoka Premier League wanamuhitaji Mfaransa huyo kwa mkopo huku Barcelona wanachohitaji wao ni kutaka kumuuza moja kwa moja kwa dau lenye thamani ya euro milioni 100.

Inadaiwa mpaka sasa uongozi wa Old Trafford akiwemo Ed Woodward wameshafanya mazungumzo na upande wa pili wa Barcelona juu ya uwezekano wa kumnasa nyota huyo.

Wakati upande wa Wakatalunya ukiweka vigezo vya lazima kumsajili moja kwa moja mara baada ya kukamilisha kuutumikia muda wake wa mkopo kuisha.

Dembele mwenye umri wa miaka 23 anaonekana kuvutiwa na mpango huo wa kutimkia English baada ya kutua Barca akitokea Borussia Dortmund kwa euro milioni 105 mwaka 2017.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *