Dewji Amfanyia Hili Shabiki wa Simba Aliyechaniwa Jezi…

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba Mo Dewji ametimiza ahadi yake ya kumtafuta shabiki wa Klabu ya Simba aliyechaniwa jezi na watani zao wa jadi, Yanga ambapo amempa jezi mpya ya klabu hiyo ya Simba.

 

Katika  kwenye ukurasa wake wa Twitter, leo Dewji ameposti picha akiwa na shabiki huyo akisema, ”Nimefurahi kukutana na wewe leo Bw. Kindio Hassan. Pole sana na changamoto uliyokutana nayo.”

 

Jana  kupitia Instagram yake aliandika, ”Namtafuta shabiki huyu wa Simba aliyechaniwa jezi, nataka kukutana naye. Mpira ni Ushindani, Mpira ni Utani, Mpira sio Uadui!”Toa comment