Dhoruba ‘CIARA’ yasimamisha mechi ya Manchester City dhidi ya West Ham

28 0

Mchezo wa ligi kuu England baina ya Manchester City dhidi ya West Ham United umeghairishwa kufuatia kuwepo kwa hali mbaya ya hewa.

Mechi hiyo ambayo ilipaswa kupigwa leo siku ya Jumapili katika dimba la Etihad, umegharishwa kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu ya Manchester City ambaye alikuwa mwenyeji wa mchezo.

Image result for Manchester City vs West Ham storm ciara

Hali mbaya ya hewa inayokwenda sanjari na dhoruba Ciara (Storm Ciara) imepelekea kugharishwa kwa mechi hiyo na nyingine baadhi huko England zilizopangwa kuchezwa leo siku ya Jumapili.

Miongoni mwa mechi nyingine iliyoathiriwa na uwepo wa hali mbaya ya hewa ni ‘Derby’ ya north London baina ya Arsenal na Tottenham kwa upande wa ligi ya Wanawake Women’s Super. Hata hivyo wale waliyokata tiketi kwaajili ya kwenda kushuhudia mechi hizo, zitakuwa zipo hai kwa michezo inayofuata.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *