Dimpoz Ampigia goti Mondi

LICHA ya kuwa na tofauti kwa muda mrefu, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ametoa kauli iliyotafsiriwa kuwa ni kumpigia goti Mbongo Fleva mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.  Dimpoz amemuomba Esma Khan ambaye ni dada wa Diamond au Mondi kufikisha ombi lake la shoo kwa kaka yake.

Akizungumza wikiendi iliyopita kwenye uzinduzi wa albam ya mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, Juma Mpangala ‘Jux’ uliofanyika kwenye Mgahawa wa Akemi uliopo Posta jijini Dar, Dimpoz alimuomba Esma kufikisha ujumbe ili naye apate shoo kwenye Tamasha la Wasafi lililo chini ya Mondi.

Dimpoz alieleza kuwa amepokea taarifa kutoka kwa daktari wake akimweleza kuwa anaweza kurudi stejini na kufanya shoo kama zamani kwa sababu ameshakaa sawa kiafya.

“Kama kuna mapromota hapa naombeni mnipe shoo maana nimepokea taarifa ya daktari kuwa sasa ninaweza kurudi stejini. “Nasikia kuna Fiesta huko inataka kuanza. Pia ninamuomba dada yangu hapo (huku akimnyooshea kidole Esma) aniombee kwenye lile tamasha (Wasafi Festival), niko tayari ku-perfom,” alisema Dimpoz.

AMPIGIA GOTI MONDI

Kutokana na kauli hiyo ya Dimpoz kwa dada wa Mondi, watu mbalimbali walianza kuichambua na kueleza kuwa mwanamuziki huyo amekubali yaishe, yaani amemaanisha kuwa amempigia magoti Mondi kwani ndiye bosi wa Wasafi Festival.

Awali Dimpoz na Mondi walikuwa marafiki walioshibana, lakini urafiki wao ulikuja kuingia doa na kuwa na bifu kali ambalo mpaka leo hawazungumzi

STORI:AMMAR MASIMBA, DAR

Toa comment