DJ SBU APAGAWA NA DJ ASHLEE WA GLOBAL RADIO

21 0

DJ Sbu ambaye jina lake kamili ni Sbusiso Leope akizindua kipindi cha ‘Afternoon Drive’ akiwa  na DJ Ashlee, mmoja wa MaDJ bora kabisa kutoka +255 Global Radio.

“NAJIONA kama nipo Sauz!” Ni maneno ya DJ maarufu kutoka Johannesburg, Afrika Kusini, Sbusiso Leope ‘DJ Sbu’ kwenda kwa DJ Ashlee wa Global Radio baada ya kupagawa kwa nyimbo za Sauz zilizokuwa zikisikika kupitia studio za +255 Global Radio.

 

DJ Sbu alitua Jumanne iliyopita ndani ya studio hizo maalum kuzindua kipindi chake kipya cha Afternoon Drive ambacho kiliruka ‘live’ kwa kushirikiana na redio yake kutoka Afrika Kusini ya Massiv Metro inayowafi kia zaidi ya wasikilizaji milioni moja kutoka Afrika.

 

Akizungumza katika kipindi hicho ambacho kitakuwa kikiruka hewani kuanzia saa 4:00 hadi 1:00 jioni kikijikita zaidi katika kuelezea tamaduni mbalimbali za vijana Afrika, DJ Sbu alianza kwa kumsifi a DJ Ashlee kuwa bado mdogo kiumri na anamuona atafi ka mbali katika kipaji chake cha kuchanganya nyimbo za Afrika Kusini.

DJ Sbu ambaye jina lake kamili ni Sbusiso Leope akizindua kipindi cha ‘Afternoon Drive’.

“Nimesikiliza mixing tangu nimekuja kutoka kwa DJ Ashlee anafanya vizuri kupiga nyimbo za Afrika Kusini nawaomba wasikilizaji wa Afrika Kusini na wote mfuatilieni kwenye kurasa wake wa Instagram, anacheza nyimbo za kwetu kama anazijua,” alisema DJ Sbu na kumtaka DJ Ashlee kueleza nani amekivumbua kipaji chake.

 

“Nakumbuka tulikutana na Borry akaniambia nijiunge naye kwenye radio hii (Global Radio), mara ya kwanza nilikataa, lakini baadaye akanitafuta tena nikasema niungane naye ndiyo nikawa hivi,” alisema DJ Ashlee.

Akiwa na watangazaji wa Bongo 255, Stewat George (kushoto), Sechelela Mazanda na Rashid Mbegani (kulia).

Baada ya kumsikia Ashlee, DJ Sbu aliendelea kusisitiza kuwa anamuona DJ huyo kufi kia mafanikio makubwa kutokana na kipaji chake. “Namuona mbali, anajua kucheza muziki vizuri na hii itamfanya kufi ka katika levo kubwa Afrika,” alisema DJ Sbu ambaye alikuwa akisaidiana kutangaza na mtangazaji ambaye pia ni meneja wa ‑255 Global Radio, Borry Mbaraka.

 

Mbali na kupagawa na Ashlee, DJ Sbu ambaye pia ni mjasiriamali, mhamasishaji, mwandishi wa vitabu akiwa ni mwanzilishi na mmiliki wa MoFaya alielezea na namna wanamuziki wa Afrika Kusini wanavyofaidika katika kazi zao za muziki.

“Upande wa wasanii wa Afrika Kusini wanafaidika sana kupitia kazi zao za muziki kwa sababu wamekuwa wakiuza nyimbo zao kupitia mitandao mingi ya kuuzia nyimbo kama Spotfy, Amazon, iTunes na mingine mingi ambayo imepelekea kazi zao kutoibiwa ovyo na wezi wa mitandao na wale wa CD kwa hiyo nawashauri wasanii wa Tanzania nao kutumia njia hiyo katika uuzaji wa kazi zao utawasaidia sana ,” alisema DJ Sbu.

 

Mahojiano kamili ya DJ Sbu unaweza kuyapata kupitia Youtube kwa kuandika Global TV Online. Pia unaweza kuendelea kusikiliza ‑255 Global Radio kwa kuipakua katika APP kwenye Playstore kupitia simu yako ya mkononi au kuingia moja kwa moja kwa kupitia www.globalradio.co.tz

ANDREW CARLOS, Dar es Salaam


The post DJ SBU APAGAWA NA DJ ASHLEE WA GLOBAL RADIO appeared first on Global Publishers.

Posted from

Related Post

Kifo Mikononi Mwangu (Sehemu ya 2)

Posted by - September 2, 2019 0
Kifo Mikononi Mwangu (Sehemu ya 2) September 2, 2019 by Global Publishers   ILIPOISHIA WIKIENDA… “Kama unakwenda kazini si ninaweza…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *