Bashiru Amuonya Kigwangalla Sakata la Simba na Mo Dewji

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru Ally, amemtaka mgombea ubunge wa Jimbo la Nzega Vijijini, Dkt. Hamis Kigwangalla, kuacha kujibizana mitandaoni kuhusu mpira na badala yake atumie muda huo kuweka vitu vitakavyomsaidia mgombea urais wa chama hicho Dkt John Magufuli kushinda uchaguzi.

 

Hayo yameelezwa jana Septemba 06,2020, kupitia ukurasa wa Twitter wa CCM, ambapo licha ya kutoa maelekezo hayo kwa Kigwangalla, pia ametoa maelekezo kwa mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye.

 

“Naona Dkt. Kigwangalla yupo mitandaoni kujibizana na Mohamed Dewji mambo ya mipira, tupo kwenye uchaguzi, nataka nione ana-tweet na wafuasi wake namna Mwenyekiti na Mgombea Urais wetu atakavyoshinda, siingilii maisha binafsi, hakuna maisha binafsi unapokuwa mgombea wa CCM,” amesema Bashiru.

 

Dkt. Kigwangalla na Mo Dewji walianza kujibishana mtandaoni baada ya Kigwangalla kuhoji namna alivyopatikana CEO mpya wa Simba ambaye anaelewa kuwa PA wa Mo Dewji.

Katika kujibu hoja hiyo Mo aliendelea hadi kumuomba msamaha Waziri Kigwangalla kutokana na mkopo wa pikipiki kutofanikiwa (hali iliyotafrisiwa kuwa Mo anadhani Kigwangalla anafanya hivyo kutokana na kunyimwa mkopo).

Hata hivyo, Kigwangalla aliendelea  kusema mkopo hauhusiki bali  yeye anahoji kama mwanachama wa Klabu ya Simba. Aliweka bayana barua-pepe aliyoombea mkopo wa pikipiki na pia alionyesha tweet zake za nyuma ambazo pia alikuwa  akihoji mambo kadhaa ndani ya Simba.Toa comment