Dkt. Bashiru Amuonya Nape: Rudi Jimboni Kwako!

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru Ally, amemtaka mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama (CCM), Nape Nnauye kurejea jimboni kwake na kufanya kampeni zitakazomsaidia mgombea urais wa chama hicho Dkt. John Magufuli kushinda uchaguzi.

 

Hayo yameelezwa  jana Septemba 06,2020, kupitia ukurasa wa Twitter wa CCM, ambapo licha ya kutoa maelekezo hayo kwa Kigwangalla, pia ameyatoa kwa mgombea ubunge Jimbo la Mtama Nape Nnauye.

 

 

Katika maelkezo hayo Dkt Bashiru amesema, “Nimemuona Nape Ilemela, wakati Jakaya kikwete anakwenda Lindi Septemba 8, 2020 kuzindua, anatakiwa awe Lindi kumuandalia Mkutano, tutakuwa wakali kusimamia nidhamu, wagombea wa CCM wapo chini ya Kamati za Siasa, lazima wafuate maelekezo, sio kujiamulia binafsi.”

 

Mbali na hayo ameongeza kuwa, “Hakuna Mgombea yeyote kutoka Jimboni kwake bila idhini ya Kamati ya Siasa ya Wilaya, tufuate ratiba za NEC na Kamati za Siasa, tuwatafutie kura wagombea Udiwani na Mgombea Urais, tufafanue Ilani yetu tuliyotekeleza na kilichobaki, na kuhamasisha wananchi kupiga kura.”

 Toa comment