Eeh! Man United wampigia simu Pochettino

7 0


MANCHESTER, England

TAARIFA kutoka katika vyanzo mbalimbali Ulaya vinasema mabosi wa Manchester United wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino.

Manchester United walikubali kichapo cha mabao 6-1 kutoka kwa Tottenham na kufanya mabosi hao kuwa na maswali mengi juu ya mwenendo wa kikosi chao tangu kuanza kwa msimu huu chini ya Ole Gunnar Solskjaer.

Kocha huyo raia wa Norway alishuhudia kikosi chake kikimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita huku wakiishia hatua ya nusu fainali kwenye Ligi ya Europa.

Lakini, tangu kuanza kwa msimu huu anaonekana kushindwa kufanya vizuri, Manchester United imeruhusu kufungwa mabao 11 katika michezo mitatu ya Ligi Kuu.

Kutokana na kiwango hicho, inaelezwa Ed Woodward alifanya mawasiliano na Pochettino ikielezwa amemwambia akae mkao wa kula, kwani Solskjaer anaweza kuondolewa wakati wowote kaa timu hiyo itaendelea kufanya vibaya.

Pochettino ambaye aliiongoza Tottenham katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019, alitimuliwa Novemba mwaka jana na alikuwa akihusishwa kutakiwa na klabu mbalimbali kubwa Ulaya.Source link

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *