Esma Afunguka Kumrudisha Tanasha Kwa Mondi

2 0Esma Afunguka Kumrudisha Tanasha Kwa Mondi

DADA wa mwanamuziki maarufu ndani na nje ya nchi, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Khan, amesema kuwa japokuwa ameolewa lakini hawezi hata siku moja kutuliza akili yake bila kutafuta chochote kwa watoto wake.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Esma alisema kuwa ameingia kwenye ndoa ikiwa ni moja ya kupata stara kwenye maisha yake kama mtoto wa Kiislam, lakini ukweli hawezi kukaa ndani tu akisubiri aletewe.

Esma alizungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti hili kama ifuatavyo:

Risasi: Vipi maisha mapya ya ndoa?

 

Esma: Mazuri sana tu.

Risasi: Juzikati hapa mlitucha nganya, kama kwamba kwenye ndoa yako kuna shida, maana mumeo aliweka wazi kuwa amemmisi mkewe mwingine…

 

Esma: Unajua shida kubwa sana ya watu, wanaangalia maisha ya mtu na kila kitu chake kwenye mitandao ya kijamii na kingine yupo mtu anakufuatilia tu akiamka toka asubuhi na kuropoka bila kuwa na uhakika.

Risasi:Unataka kutuambia hamkuwa na tofauti zozote?

Esma: Mimi sina shida na mume wangu wala hakuna kilichotokea, watu waache tu kukariri maisha mtandaoni, maana hawajui kama hata huyo mama Melo ni nani, ndugu yake au vipi.

Risasi: Esma wewe ni mama wa watoto wawili, ni vipi unawalea watoto wako?

Esma: Watoto wangu nawalea kawaida sana, lakini kikubwa pia nawalea kwenye maadili ya dini.

Risasi: Watoto wako wamezaliwa kwenye familia ya staa, je malezi yao ni tofauti na watoto wengine?

 

Esma: Hapana, watoto wangu wote kwa kweli wanaishi maisha ya kawaida sana kama ilivyo kwa wengine na ninapenda hivyo kwa sababu hata mimi nililelewa maisha ya kawaida tu.

 

Risasi: Wengi wanaamini kwa vile kwa upande wa nyumbani kwenu mko vizuri kifedha, na hata kwa mumeo pia, watu walijua ungeacha hata kuendelea na biashara unayofanya.

Kwa nini bado unakomaa?Esma: Siwezi kubweteka hata kidogo, hata kama ningeolewa na bilionea wa dunia, lazima ningeangaika huku na kule.

 

Risasi: Hivi karibuni niliona unampost mtoto wa Tanasha na kuweka wazi kuwa unamkumbuka, sasa kwa upande wako hujaweza kurudisha mahusiano ya Diamond na Tanasha kama wifi ?

 

Esma: Kila siku nasemaga mapenzi hayaingiliwi hata kidogo, na mimi kila siku naheshimu kile kaka yangu anakiona kwa sababu najua wazi ana sababu zake kama amefanya kitu, na pia watoto wa Diamond ni damu yangu kabisa, hivyo nawakumbuka sana tu.

 

Risasi: Nasikia tayari ndoa imejibu na ndiyo maana hauonekani sasa hivi mara kwa mara.Esma: Hiyo ni siri yangu, kama ipo itaonekana maana siwezi kufi cha tumbo, lazima likue na kuonekana.

Risasi: Taraji anaonekana anampenda sasa baba yake Petitman, vipi anawezaje kukaa hivyo bila baba yake?

 

Esma: Anaonana na baba yake, hilo halina tatizo kabisa.

 

Risasi: Nini ambacho umekipanga juu ya watoto wako?Esma:Hakuna kitu kizuri kana uwepo wangu kwao, lakini kingine kikubwa nikiwapa elimu ya kutosha, naona ndiyo kitu ambacho watafurahi kutoka kwangu.

 

Risasi: Watoto wako wanapokosea, unawafanyaje?

 

Esma: Kwanza mimi sipendi kupiga watoto, lakini ukweli ni kwamba, nazungumza nao tu wananielewa, maana naona hata nikiwapiga ni kama nawakomaza tu.Risasi: Kulea hivi watoto wenyewe bila baba zao, huoni kama kuna kitu unakimisi kutoka kwa baba zao?

Esma: Labda kwa upande wao na pia kila mama anapenda sana kulea watoto wake pamoja na baba zao, lakini inapotokea kuwa mbalimbali inabidi tu, na uzuri mume wangu anapenda sana watoto, hilo ni jambo la kumshukuru sana Mungu.

Risasi: Unapenda watoto wako waje kuwa wakina nani baadaye?

Esma: Unajua mimi sipendi kuwachagulia, ila najua kila mtoto ana kipaji chake, mimi nitafuata kile wanachopenda wenyewe.

Risasi: Unapata muda gani wa kuwa nao, maana muda mwingi unakuwa dukani.

 

Esma: Mara nyingi wakitoka shule wanakujaga hapa dukani na kuna wakati anakuwa dukani mtu mwingine na mimi nabaki nao kwa muda mrefu.

Risasi: Wengi wanafi kiri kuwa kwa sababu watoto wako wamezaliwa kwenye familia ya staa mkubwa, basi wangekuwa wanaonekana sehemu tofauti kama ilivyo kwa mastaa wengine, unazungumziaje hilo?

Esma: Unajua hata kama mtoto amezaliwa katika familia ya mastaa kiasi gani, kikubwa ni kuangalia mambo ambayo mtoto anapaswa kuyafuata na si kingine.Risasi:Haya Esma asante sana kwa ushirikiano.Esma:

MAKALA: IMELDA MTEMA , RISASIToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *