Fahamu jinsi mapenzi ya Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe, yalivyoitikisa Zimbabwe wakati wa uhai wake

15 0

Katika Umri wake mkubwa wengi walidhania kwamba aliyekuwa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe angekuwa akikabiliwa na upungufu wa fahamu, lakini kama mvinyo, alikuwa akionekana kuimarika kila uchao.  Uhusiano wa kimapenzi kati yake na mkewe Grace Marufu ulianza wakati alipokuwa akifanya kazi kama mpiga chapa katika ikulu ya rais ya Zimbabwe .

Wawili hao walianza kuonana kisiri wakati Mugabe alipokuwa na mkewe wa kwanza Sally ambaye alikuwa akiugua, tofauti ya umri wao ikiwa miaka 40.

‘Alikuja kwangu na kuanza kuniulizia kuhusu familia yangu”, alisema Grace Mugabe katika mahojiano kuhusu walivyojuana na kiongozi huyo miaka ya 80.

”Nilimuona kama babaangu. Sikudhania kwamba atanitazama na kuniambia nampenda huyu msichana, sikutarajia hata kidogo”, aliongezea bi Grace akizungumza na BBC.

Ijapokuwa bado alikuwa na mkewe wa kwanza Mugabe hakuweza kuzuia mapenzi tele ya Grace, alisema akihojiwa na vyombo vya habari nchini Zimbabwe.

”Mamangu alikuwa akilia akisema kwamba angependelea kuwaona watoto wangu kabla ya kufariki, Mugabe alinukuliwa na chombo cha habari cha NewsdzeZimbabwe.

”Mke wangu Sally alikuwa mgonjwa na alikuwa kitandani na wakati huo nikakutana na Grace katika ikulu ambapo alikuwa akifanya kazi kama katibu wangu”, alinukuliwa akisema.

”Ni kweli tulianza uhusiano huo wakati Sally alipokuwa hai” , ilinibidi.

”Mimi na Grace hatukuchumbiana, nilijulishwa kumuhusu na nikajiambia ni msichana mrembo” .

Grace Mugabe

”Hivyobasi alianza kufanya kazi kama katibu na walikuwa wengi katika Ikulu, niliwatazama na hapo mapenzi yakaanza tulipoonana na Grace”.

Aliongezea: Na baadaye , siku moja nilimwambia, nakupenda na nilimuona ameshikwa na ganzi. Nilimshika mkono wake na kumpiga busu.

”Hakukataa na wala kupinga na baadaye nikaambia nafsi yangu kwamba kwa kuwa amekubali busu langu basi nimemaliza mchezo”. alinukuliwa na vyombo vya habari vya Zimbabwe akisema.Mugabe alisema kwamba wawili hao walikuwa wakikutana kisiri katika nyumba ya dadake marehemu Sabina huku wapwa wake wakitumwa nje ili kuficha uhusiano huo.

Bwana Mugabe anasema kwamba mkewe wa kwanza Sally aliupatia baraka uhusiano wake na Grace kabla ya kifo chake 1992.

Hatahivyo anasema kwamba hakumuoa Grace hadi miaka minne baadaye.

Wapenzi hao wawili walipata watoto watatu: Bona, Robert na Chatunga.

Licha ya wengi kudai kwamba alikuwa akikabiliwa na saratani ya tezi dume , Bwana Mugabe aliishi maisha yenye afya .

Kwa mujibu wa BBC. Grace alinukuliwa akisema kwamba {Mugabe} alikuwa akiamka saa kumi na moja alfajiri ili kufanya mazoezi ya maungo ikiwemo Yoga na kwamba mumewe hakunywa pombe ama hata kahawa na mara nyingi alipendelea kula mboga

Kabla ya hotuba zake Mugabe alikuwa akimpiga busu la chini ya kidefu chake mkewe Grace ili kuonyesha upendo wake kwake.

Na kufuatia mapenzi hayo Bi Grace naye hakuachwa nyuma kwani aligonga vichwa vya habari mara kwa mara kwa kumuunga mkono mumewe kwa kila jambo.

Bi Grace Mugabe na Mumewe marehemu Robert Mugabe

Alizua gumzo nchini Zimbabwe wakati mmoja aliposema kwamba mumewe anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti.

Alisema kwamba jina lake litawekwa kwenye karatasi za kupiga kura hata akiaga dunia mbali na kutumia uongozi wa mumewe kuwakabili wapinzani wake mara kwa mara.

Hatahivyo alizua songombigo wakati wa mwisho mwisho wa uongozi wa Robert Mugabe alipomtaka mumewe kumtaja ‘mrithi’ wake ili kupunguza migawanyiko kuhusu mtu atakayemrithi..

”Rais hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno lake litakuwa la mwisho”,alisema bi Grace Mugabe.

Na wakati alipohisi kwamba mambo yalikuwa yanaenda mrama katika kambi ya kisiasa ya mumewe bi Grace hakusita kuonya kwamba kulikuwa na uwezekano wa kufanyika kwa mapinduzi nchini humo huku kukiwa na uvumi kwamba huenda Mugabe akamwachia mkewe uongozi wa taifa hilo.

By Ally Juma.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *