fahamu: Utafiti waonyesha sumu ya nyuki ina uwezo wa kutibu saratani ya matiti

11 0

Wanasayansi wa Australia wanasema kwamba sumu ya nyuki wanaotengeneza asali ina uwezo wa kuharibu seli hatari za saratani ya matiti katika maabara.

Sumu hiyo na kemikali aina ya melitin – zilitumika dhidi ya aina mbili ya saratani ambazo ni ngumu kutibu.

Ugunduzi huo umetajwa kuwa wa kufurahisha , lakini wanasayansi wametoa tahadhari kwamba vipimo zaidi vinahitajika.

Saratani ya matiti imeelezewa kuwa saratani ambayo inawaathiri wanawake wengi duniani.

Huku kukiwa na maelfu ya kemikali zinazoweza kukabiliana na seli za saratani katika maabara, wanasayansi wanasema kwamba kuna chache zinazoweza kuzalishwa kama tiba ya wanadamu.

Sumu ya nyuki awali ilibainika kuwa na tiba dhidi ya aina nyengine ya saratani kama ile ya Melanoma.

Utafiti huo wa taasisi ya Harry Perkins kuhusu tiba magharibi mwa Australia ulichapishwa katika jarida la asilia.

Je utafiti huo uligundua nini?

Ulifanyia vipimo sumu za nyuki 300. Sumu hizo kutoka kwa nyuki wa kutengeneza asali zilionekana kuwa na uwezo mkubwa, alisema Ciara Duffy, mtafiti wa umri wa miaka 25 ambaye aliongoza utafiti huo.

Sumu hiyo kali iligunduliwa kuwa na uwezo wa kuuwa seli za saratani ndani ya saa moja, bila kudhuru seli nyengine.

Lakini sumu hiyo iliongezeka viwango vingine vya tiba.

Dr Ciara Duffy
 

Utafiti huo pia ulibaini kwamba kemikali ya Melittin kivyake ilikuwa na uwezo mkubwa katika kuuwa au kuharibu ukuaji wa seli za saratani.

Huku Melittin ikiwa ndani ya sumu ya nyuki wa asali pia inaweza kuzalishwa katika maabara.

Je inaweza kutumika katika siku za usoni?

Siku ya Jumatano, wanasayansi kutoka Australia magharibi walielezea utafiti huo kama wa kufurahisha.

Muhimu, ni kwamba utafiti huu unaonesha kwamba Melittin inaingilia ukuwaji wa seli za saratani ndani ya matiti ili kuzuia kuzaana kwa seli hizo , alisema Profesa Peter Klinken.

“Inatoa mfano mzuri wa ni wapi kemikali asilia zinaweza kutumika kutibu ugonjwa unaoathiri wanadamu.

Lakini watafiti hao wanaonya kwamba kazi zaidi inahitajika kuona iwapo sumu inaweza kutumika kwa kiwango gani kama tiba ya saratani.

Unaweza pia kusoma:

Watafiti wengine wa saratani wanakubali kwamba ni mapema mno, alisema profesa Alex Swarbrick kutoka taasisi ya tiba ya Sidney.

Kemikali nyingi zinaweza kuuwa saratani ya matiti katika panya. Lakini kuna mengi ya kufanywa kutoka katika tafiti hizo hadi kufikia kiwango ambacho kinaweza kubadili tiba ya ugonjwa huo.

Chanzo BBC.

Posted from

Related Post

IN SHA ALLAH

Posted by - October 27, 2019 0
ASHA KIGUNDULA NA JESSCA NANGAWE VITA ya kibabe ya soka itakayowakutanisha Yanga dhidi ya Pyramids ya nchini Misri inatarajiwa kushuhudiwa…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *