Fomu ya Urais kuanza kutolewa leo makao makuu ya NEC Dodoma

17 0

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, hivi karibuni inaonesha kwamba, wagombea Urais wenye nia ya kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanatakiwa kufika Njedengwa jijini Dodoma kuanza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo.

Fomu za Urais zitachukuliwa kwa muda wa siku 20 kati ya Agosti 5 hadi Agosti 25, mwaka huu na watu wenye sifa ya kugombea nafasi ya kiti cha Urais ambao watakuwa wameteuliwa na vyama vyao vya siasa vyenye usajili wa kudumu ndiYo watakaofuata fomu hizo.

Mpaka sasa hivi vyama vilivyopitisha wagombea wa nafasi hiyo ni, Chama cha Mapinduzi ambacho kimempitisha Rais Magufuli, chama cha CUF kimemteua Profesa Lipumba, CHAUMA atasimama Hashim Rungwe, John Shibuda ataiwakilisha TADEA, huku CHADEMA kiti hicho kikitetewa na Tundu Lissu.

Chanzo Eatv.tv

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *