Gigy: Nalipa Kodi Milioni 4 kwa Mwezi

Staa wa kike wa Bongo Fleva Gigy Money amefunguka kuwa ana pesa za kumlisha miaka ijayo hata kama asipofanya kazi, pia amesema analipa kodi ya milioni nne kwenye nyumba yake.

 

Gigy Money amesema pesa hizo anajilipia mwenyewe tena bila ya kudanga au kutumia pesa ya mwanaume.

 

“Mimi ninafanya kazi zangu na najituma hakuna hata mwanaume nyuma yangu msije mkajidanganya kama nadanga, ninalipa kodi ya Milioni nne kwa mwezi, mimi sio mwanamuziki pekee bali ni mburudishaji, nina ushawishi na balozi nina pesa ambayo nimelipwa na zinaweza kunilisha miaka,” amesema Gigy MoneyToa comment