GNM: Licha ya Corona, Tunaendelea Kusafirisha Mizigo Kutoka China

32 0

GNM: Licha ya Corona, Tunaendelea Kusafirisha Mizigo Kutoka China

UCHUMI wa dunia nzima ni kama umesimama! Biashara nyingi zimefungwa, wafanyabiashara wanahofia kusafiri kwenda China kufuata bidhaa mbalimbali, serikali za nchi mbalimbali nazo zimeweka zuio la safari za nje zisizo na ulazima na kusababisha hali izidi kuwa mbaya kwa wafanyabiashara.

 

Hata hivyo, kama wewe ni mfanyabiashara na hutaki mambo yako yasimame na hutaki kupoteza mtaji wako, GNM Cargo inakupa fursa ya kuendelea na shughuli zako za kuagiza bidhaa mbalimbali ukiwa nyumbani katika kipindi hiki ambacho Corona ni tishio duniani kote.

 

GNM Cargo wanakuwezesha kuagiza mzigo wowote unaoutaka kutoka China, kuanzia nguo, pochi za kisasa, vifaa vya simu, viatu, spea za magari na pikipiki na vitu vingine vingi bila ulazima wa wewe mwenyewe kusafiri, tena kwa bei rahisi kabisa.

 

Kuagiza na kusafirisha belo (bale) kubwa la nguo la CBM 1, boksi kubwa la nguo au spea za magari kutoka China mpaka Dar es Salaam Utalipia dola Kimarekani 400 (sawa na takribani shilingi laki tisa na elfu ishirini tu).

 

Kwa vifurushi vya mikoba, viatu na vifaa vya nguo utalipia dola za Kimarekani 350 ambazo ni sawa na shilingi laki nane, kwa spea za pikipiki utalipia dola 300 ambazo ni sawa na shilingi laki sita na elfu tisini tu, viwango ambavyo ni nafuu sana ukilinganisha na kama ungesafiri mwenyewe, au kama ukilinganisha na kampuni nyingine zinazosafirisha mizigo kutoka China.

 

Unachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na ofisi za GNM Cargo zilizopo Tanzania na China na kuwaeleza mzigo unaoutaka kisha wao watakufanyia kila kitu na kazi yako itakuwa ni kusubiri mzigo wako ambao utaletwa mpaka mlangoni kwako.

 

Hiyo itakurahisishia kuendelea na shughuli zako kama kawaida bila kuwa na hofu ya ugonjwa wa Corona na kukwepa usumbufu uliopo hivi sasa ambapo haiwezekani kwa mtu asiye na sababu maalum kuruhusiwa kusafiri kuingia au kutoka China.

 

Namna ya kuwasiliana na GNM Cargo ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kufika kwenye ofisi zao zilizopo Kariakoo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Msimbazi, Mkabala na Benki ya Azania na Jengo la Simba Sport Club, ghorofa ya tatu au unaweza kuwapigia simu kwa namba 0677 066 551, 0677 066 555 au 0677066556 kwa Tanzania.

Kwa nchini China ofisi zao zipo Guangzhou na namba ya kuwasiliana nao ni +8613143709658. Pia unaweza kuwasiliana nao kwa WhatsApp kwa namba zote za hapo juu au watumie barua pepe kwa anuani za info@gnmtrading.com na gnmtradco@yahoo.com.

 

GNM Cargo pia inakukumbusha ewe mteja kuchukua tahadhari zinazoelezwa na mamlaka husika kuhusu kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Makala: MWANDISHI WETU, DAR
Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *