Gonjwa Linalomtesa Mbosso!

Staa mwingine wa Bongo Fleva anayetumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Mbwana Yusuph Kilungi ‘Mbosso Khan’ amekiri kuteswa na gonjwa baya la kutetemeka. Mbosso amesema kuwa, ugonjwa huo umekuwa ukimsumbua tangu akiwa mtoto mdogo.

 

Mbosso amesema; “Ni kweli naumwa, mimi nina matatizo ya mikono, siwezi kunyoosha mikono.

 

“Ni ugonjwa ambao niko nao tangu nazaliwa, nakumbuka kipindi nakua nimeshavunja sana vitu. Nakumbuka kipindi cha kwanza naingia Mkubwa na Wanawe (Yamoto Band) hata viongozi wangu wakawa wanahisi labda natumia vitu ambavyo siyo vizuri.”

 

Mbosso ameongeza; “Hii hali inanijia tu, inaweza kukaa kwa muda kisha ikaniacha, lakini mara nyingi inaishi kwenye maisha yangu.”

Stori: Khadija bakari, DarToa comment