Harmonize agawa magari kwa wasanii wake

1 0

Msanii wa muziki wa bongo fleva Harmonize na CEO wa Konde Gang Music amemtangaza rasmi msanii wa Hip hop Ibrahim Mandingo maarufu kama Country Boy ambaye amejiunga na kundi hilo.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari Harmonize amewazawadia wasanii wake ambao wapo katika lebo ya Konde Gang kila mmoja gari aina ya Crown.

Itakumbukwa mapema wiki hii kundi hilo liliwatambulisha wasanii Ally kili Omary maarufu kama Killy na Rashid maarufu kama Cheed waliotoka katika kundi la Kings Music, ambapo usiku wa leo septemba 11, 2020 kutakuwa na ‘show’ itakayo fanyika makao makuu ya Konde Gang. 

Kwa sasa kundi hilo lina jumla ya wasanii sita ambao ni Harmonize, Ibraah, Young Skales, Killy Cheed pamoja na Country Boy.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *