Harmonize Aitumia Yanga SC Kumjibu Diamond

STAA wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ amemlipa aliyekuwa bosi wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya juzi Jumatatu kuachia wimbo maalum wa klabu ya Yanga ukiwa na mahadhi ya Singeli.

Harmonize ametunga wimbo huo ukiwa maalum kwa ajili ya Yanga kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi ikiwa ni siku chache baada ya Diamond kutoa wimbo wa Simba ambao aliupafomu katika kilele cha Simba Day.

Hadi kufikia jana Jumanne wimbo huo wa Harmonize ulikuwa namba saba kwenye video ‘zilizo-trend’ katika mtandao wa YouTube huku ukiwa na watazamaji 132,422 baada ya kupostiwa Agosti 24.

Pia wimbo huko ulikuwa umepata likes 10,000 na dislike 872, ambapo mashabiki wengi ambao walitoa maoni katika wimbo huo walikuwa wakiupongeza.Hata hivyo, akiwa kwenye makao makuu ya Yanga jana, Harmonize alisema kuwa mshabiki wategemee shoo kali siku ya kilele cha Mwananchi na kuwa shabiki wa Yanga siyo dhambi.

 

“Mimi kuishabikia Yanga siyo dhambi wala siyo ugomvi, siamini kama mtu akiishabikia timu itampunguzia mashabiki, ninachofahamu michezo siyo uadui ni furaha na urafiki,” alisema Hamonize, jana.

Simba na Yanga zipo katika mbio za kuusaka ubingwa katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 ambapo kila upande umeonyesha kujiimalisha katika usajili ili kuleta ushindaniToa comment