Harmonize Amjibu Diamond “Wewe SIMBA Mimi ni TEMBO”

VITA ya panzi majani ndiyo yanayoumia! Unaweza kutumia msemo huu kutokana na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ kuonekana akiwa amechora tattoo ya tembo mgongoni na kuzua balaa kwa kile wengi walichodai kuwa amemjibu Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye ana tattoo ya simba.

 

Harmo alizua balaa la aina yake baada ya picha yake hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram ambapo wengi waliyoiona walidai kuwa amemjibu Diamond kwamba yeye ni tembo ambaye ni mkubwa kuliko simba.

 
Toa comment