Hatimaye Lamine Moro mali ya Yanga hadi 2023

BEKI wa kimataifa wa Yanga, Lamine Moro leo Septemba 29, 2020 ameongeza mkataba wa kuwatumikia mabosi wake Yanga hadi mwaka 2023.

Lamine, raia wa Ghana hivi karibuni iriripotiwa kuwa mkataba wake unakaribia kufika ukingoni jambo ambalo limewafanya mabosi wake kumpa dili jipya kutokana na uwezo wake kuwa ndani ya uwanja.

Lamine amesema:-“Ni kweli nimeona vyema kuongeza mkataba, kwanza itanipa muda zaidi wa kutekeleza majukumu yangu.”

Beki huyo kisiki alijiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bidcom ya Zambia mkataba ambao unamalizika mwishoni mwa msimu ujao 2021. Lamine ataendelea kubaki mitaa ya Jangwani hadi Julai 2023.
Ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa amecheza mechi tatu na amefunga mabao mawili.
Toa comment