Humoud: Yanga? Mbona Freshi Tu

KIUNGO wa kati wa Mtibwa Sugar, Abdulhalim Humoud, ameweka bayana kuwa anajisikia furaha kusikia kuwa anahusishwa na kujiunga na Yanga kutokana na ukubwa wa timu hiyo hapa nchini.

 

Ikumbukwe Humoud katika mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar na kumalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0, baada ya mchezo huo alionekana akiwa amevaa jezi ya Yanga na kwenda kupiga picha na mashabiki wa timu hiyo ambao walimshangilia.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Humoud alisema kuwa, yeye kuhusishwa kujiunga na Yanga kwake anajisikia faraja kubwa kwa kuwa Yanga ni timu kubwa pia yeye ni mfanyakazi na mpira ndio kazi yake, hivyo atajisikia pia furaha kucheza kwenye timu kubwa.

“Kuhusu tetesi za mimi kutakiwa na Yanga najisikia faraja sana kwa kuwa Yanga ni timu kubwa sana hapa nchini, na kama ambavyo unafahamu hakuna mfanyakazi ambaye hapendi kufanya kazi sehemu kubwa na mimi ni mfanyakazi, hivyo napenda kufanya kazi sehemu kubwa.

 

“Kwa sasa nipo Mtibwa Sugar, naishi vizuri na nayafurahia maisha ya hapa, hivyo ni ngumu kusema kuwa nataka labda kuondoka Mtibwa baada ya msimu huu kumalizika, tusubiri muda utaongea,” alisema kiungo huyo.
Toa comment