Husna Maulid Achekelea Kulea

TOFAUTI na wengi huwa wanadai kulea ni kazi ngumu, kwa mrembo ambaye amewahi kushiriki Miss Tanzania aliye pia video queen, Husna Maulid kwa upande wake ameeleza kuwa ni mazuri hakuna ugumu wowote.

 

Akibonga na Amani, Husna alisema maisha ya kulea ni mazuri na hayana ugumu kama wengi wanavyodai, bali yanaongeza furaha ndani ya nyumba.

“Maisha ya kulea ni mazuri sana na kuwa na mtoto ni raha asikwambie mtu, maana hata kama nimenuna, nikimwangalia mwanangu hivi najikuta nikitabasamu tu kila wakati, namshukuru Mungu sana kwa kunipa mtoto,” alisema Husna.
Toa comment