Innocent “Mtoto mkubwa wa mke wangu ananizidi miaka 6 na ndio anayenikubali sana na kufurahia mimi kumuoa mama yake” – Video

25 0

Innocent Nyange mwenye umri wa miaka 24 mzaliwa wa Tanga kabila mzigua amemuoa Gokeys, Dokeys mwenye umri wa miaka 62 mzaliwa wa Kigoma kabila muha, Bibi huyo mwenye watoto wawili na akiwa muimbaji nyimbo za Injili, alieleza kuwa alifiwa na mumewe miaka 20 iliyopita.

Wakiongea na Bongo5 Wanandoa hao wameeleza jisi wanavyotaka kubadilisha baadhi ya amwazo ya watu kuwa kijna wa kiume kuoa mwanamke aliyemzidi umri ni kosa, Mbali na hilo Innocent ambaye ndio mume ameeleza kuwa mtoto wa kiume wa mama huyo  ambaye anamiaka 30 ndio anayemkubali na mara nyingine huwa wanashauriana kuhusu mamabo ya kimaisha.

Mbali na hilo Gokeys Dokeys amewataka wanawake wote Tanzania na duniani kote kumheshimu mume hata kama ni kipofu lakini pia wawe na mapenzi ya kweli na kuzidisha maombi kwa mungu ili awape wepesi katika kuziendesha ndoa zao.

By Ally Juma.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *