Inzi amponza mwenye nyumba – Bongo5.com

3 0

Mwanaume mmoja nchini Ufaransa amejikuta akiunguza sehemu kubwa ya nyumba yake baada ya kutaka kumuua Inzi aliyekuwa akimsumbua.

Mtu huyo ambaye ana umri wa zaidi ya miaka 80 alijikuta akiunguza nyumba yake kwa kutaka kumuua Inzi huyo ambaye alikuwa anamsumbua kwa kelele alipokuwa anakula kwa kutumia kifaa cha umeme cha kuulia mende.

Tukio hilo limetokea siku ya Ijumaa jioni alipokuwa akila chakula cha usiku ndipo alipotokea Inzi huyo na kuanza kumpigia kelele.

Aliamua kuchukua kifaa cha umeme kilichotengenezwa kwa ajili ya kuwauwa mende akaanza kumuua nzi huyo lakini kwa bahati mbaya gesi ilikuwa inavuja katika nyumba iliyopo kando ya mto Dordogne nchini Ufaransa.

Gesi na kifaa chake vilisababisha mlipuko na sehemu ya paa la nyumba yake iliyopo katika kijiji cha Parcoul-Chenaud ikaharibika.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini humo, mwanaume huyo ambaye hakuwa na silaha alibahatika kutoroka akiwa ameungua katika sehemu ya mkono wake. Huku hatma ya Inzi huyo bado haijajulikana, chombo cha habari cha Sud-quest kilisema.

Mwanaume huyo kwa sasa amejihifadhi katika hoteli moja ya eneo hilo huku familia yake ikikarabati nyujmba yake.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *