Iran yaukosoa Umoja wa Falme za Kiarabu kurejesha uhusiano na Israel

1 0

Rais wa Iran Hassan Rouhani amezikosoa Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kurejesha uhusiano na Israel.

Rouhani amezitaja nchi hizo kama watumwa wa Marekani ambao viongozi wao wanatishia usalama wa ukanda mzima wa Mashariki ya kati.

Matamshi yake haya aliyoyatoa kupitia taarifa yanakuja baada ya UAE na Bahrain kutia saini makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Israel hapo jana. Tukio hili lilifanyika katika ikulu ya White House mbele ya Rais Donald Trump.

Kwa sasa kuna jumla ya nchi nne za Kiarabu ambazo zina uhusiano wa kidplomasia na Israel zikiwemo Misri na Jordan.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *