Jamaa Mwenye ‘Sura Mbaya’ Zaidi Duniani, Aoa Mke wa Tatu

Katika njia nyingine ya kuthibitisha kuwa mapenzi ni upofu, Mchekeshaji maarufu nchini Uganda, Godfrey Baguma almaarufu kama ‘Ssebabi’, ambaye hutambulika kama mwanaume mwenye sura mbaya zaidi duniani, ameoa mke wa tatu.

 

Baguma (47), aliandaliwa sherehe ya kukata na shoka na barafu wake wa moyo, huku wawili hao wakionekana kujaa tabasamu kwenye nyuso zao katika picha ambazo zimesambaa kwenye mtandao wa kijamii.

Mchekeshaji huyo, alishinda taji la watu wasiojiweza mwaka 2002, baada ya kushiriki mashindano hayo ili kusaidia familia yake kupata chakula.

 

Baguma ambaye anaaminika kuwa na changamoto za kiafya zisizojulikana, alimuoa mke wake wa pili aliyefahamika kwa jina la Kate Namanda, mwenye miaka 30 na kujaaliwa watoto sita.

Kabla ya kufunga pingu za maisha na Kate mwaka 2013, Baguma alikuwa amejaaliwa watoto wawili na mke wake wa kwanza, lakini ndoa hiyo haikudumu baada ya kumfumania na mwanaume mwingine.

 

Mchekeshaji huyo alibandikwa jina la Ssebabi, baada ya kushinda mashindano ya mwanaume mwenye sura mbaya zaidi duniani, na kwa sasa ni baba ya watoto saba.

Stori | MWANDISHI WETU na MitandaoToa comment