Japan Yajaribia Gari Linalopaa Kama Ndege

KAMPUNI la Sky Drive Inc. lilifanya onyesho Agosti 25, 2020, eneo la  Toyota Test Field, ambalo ni moja ya makampuni makubwa zaidi nchini Japan, na likiwa ndiyo makao makuu ya magari ya aina hiyo.  Onyesho hilo lilikuwa la gari lenye kupaa, jambo ambalo lilikuwa la kihistoria nchini humo.

 

Gari hilo lililopewa jina la SD-03, likiwa na rubani, lilipaa angani na kulizunguka eneo hilo kwa dakika nne.

“Tumefurahi sana kutengeneza gari la kwanza lenye kupaaa nchini Japan tangu tuanzishe kampuni la SkyDrive… lengo likiwa ni kukiingiza kwenye biashara chombo hiki,” alisema Mtendaji Mkuu  Tomohiro Fukuzawa, katika taarifa.

 

 

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, SD-03 ndilo gari dogo zaidi duniani lenye kuondoka kwa kupaa juu moja kwa moja na ukubwa wake ni sawa na magari madogo mawili yakiwa pamoja na lina mota nane za kuhakikisha usalama wakati wa matatizo ya dharura.

 

Kampuni hilo linatumaini  kulifanya gari hilo kuwa moja ya vitu vya kawaida na si chombo cha biashara tu.    Majaribio zaidi ya kulipaisha gari hilo  yatafanywa siku zijazo na kuhakikisha usalama na teknolojia yake kuenda sambamba na viwango vinavyotakiwa.

 

Mafanikio ya jaribio hilo yanamaanisha gari hilo litajaribiwa nje ya eno la Toyota mwishoni mwa mwaka. Pia, kampuni litaendelea kuimarisha teknolojia kuhusu usalama wa gari hilo mnamo mwaka 2023.  Bei ya gari hilo bado haijatajwa.Toa comment