Jeff Bezos alivyovunja rekodi nyingine ya kuwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 200

2 0

Jeff Bezos tayari alishakuwa mtu tajiri zaidi duniani. Na sasa ameongeza tena thamani ya utajiri wake, akiweka rekodi nyingine mpya.

Siku ya Jumatano, utajiri wa mmiliki huyo wa Kampuni ya Amazon ulifikia thamani ya dola za kimarekani bilioni 202, kwa mujibu wa orodha ya mabilionea iliyotolewa na Bloomberg, wakati huu ambapo hisa za kampuni ziliongezeka, mpaja dola bilioni 87 tangu mwezi Januari Shirika la habari la CNN limeripoti.

Bezos, ambaye alianzisha kampuni ya Amazon mwaka 1994, amekuwa akiweka rekodi kutokana na utajiri wake. Mwaka 2017, alikuwa mtu tajiri zaidi duniani. Na mwezi uliopita, karibu thamani ya dola bilioni 172, akiwema rekodi mpya kubwa duniani.

Bilionea huyu hayuko peke yake- watu wengine nguli katika masuala ya teknolojia wamekuwa wakiongeza thamani ya utajiri wao wakati wote wa janga la virusi vya corona, kwa kuwa kulikuwa na ongezeko la uhitaji mkubwa wa bidhaa na huduma.

Jeff Bezos na Elon Musk
Maelezo ya picha,Jeff Bezos na Elon Musk

Mapema mwezi huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg aliitwa “centibillionaire,” kwani utajiri wake ulizidi dola bilioni 100. Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla (TSLA) Elon Musk, akiwa na jumla ya thamani ya dola bilioni 96, yuko karibu kufanikisha kiwango hicho.

Mwanzilishi wa Microsoft (MSFT) Bill Gates tayari amefanikiwa kufikia kiwango hicho.

Mkurugenzi mtandaji wa Apple( AAPL) Tim Cook pia alitangazwa bilionea hivi karibuni baada ya hisa za kampuni yake sasa kuwa na thamani kubwa zaidi- zimepanda.

Jeff Bezos Mtu tajiri zaidi duniani
Maelezo ya picha,Jeff Bezos Mtu tajiri zaidi duniani

Ingawa Amazon ndio sababu kubwa kwa Bezos kuweka rekodi , si kampuni pekee anayoiangalia. Nje ya Amazon, Bezos pia anamiliki , kampuni ya Blue Origin , inayofanya safari za anga za mbali aliyoianzisha mwaja 2000, na Gazeti la The Washington Post, ambayo aliyopata mwaka 2013.

Mwaka jana, Bezos na aliyekuwa mkewe MacKenzie Scott, zamani MacKenzie Bezos, alitangaza kuachana kwao. Ambako kulipelekea kupata robo ya hisa za Amazon.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *